Thursday, October 26, 2017

AUDIO:BRACKET FT KOREDE BELLO - JUST LIKE THAT



NEWS:LULU AKUTWA NA HATIA YA KUUA BILA KUKUSUDIA,HUKUMU YAKE KUTOLEWA NOVEMBA 13

Kesi inayomkabili muigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo alhamisi imeendelea kusikilizwa Mahakamani ambapo washauri watatu wa Mahakama kuu wamesema mshitakiwa Lulu aliua bila ya kukusudia.
Baada ya kusikiliza maoni ya baraza la wazee leo Mahakama kuu ya tanzania, imesema Elizabeth Michael amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia, muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake na hukumu yake itatolewa Novemba 13.
Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.
Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa.

VIDEO:QBOY MSAFI FT MR BLUE[Byser] - KAMOYO



VIDEO:KCEE FT SAUTI SOL - WINE FOR ME



VIDEO:MWANA FA,AY & FID Q - UPO HAPO EXTENDED

https://cloudup.com/files/ietSeBgmIrA/download

AUDIO:MC GALAXY - PLANTAIN



NEWS:MAHAKAMA YAWAPA USHINDI TENA MWANA FA NA AY DHIDI YA TIGO

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinyijuma na Ambwene Yesaya wameendelea ‘kuigaragaza’ mahakamani kampuni huduma za simu za mkononi ya Tigo, baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala kutupilia mbali maombi yake.
Kampuni hiyo ilikuwa ikiiomba mahakama hiyo iamuru kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, ijumuishwe kwenye hukumu hiyo, kama mmoja wa wadaiwa, kwenye hukumu ya Mahakama hiyo iliyoiamuru kuwalipa wasanii hao fidia ya Sh2.1 bilioni.
Hata hivyo jana Jumatano mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi hayo baada ya kukubaliana na hoja za wasanii hao kupitia kwa wakili wao, Albert Msando kuwa utaratibu walioutumia kutoa maombi hao sio sahihi.
Katika maombi hayo, Tigo walikuwa wakiomba mahakama hiyo iamuru kampuni hiyo ijumuishwe kwenye hukumu hiyo chini ya kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, wakidai kuwa kampuni hiyo pia ina hoja za kujibu.
Tigo ilikuwa inadai kuwa Cellulant ndio iliyowapelekea nyimbo hizo na kwamba yenyewe haikujua kama kampuni hiyo haikuwa na makubaliano na wasanii hao.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, wasanii hao kupitia kwa wakili wao walipinga madai hayo wakidai kuwa kifungu walichokitumia hakitoi mamlaka kwa Mahakama kumuongeza mdaiwa mwengine kwenye kesi ambaye hakuwepoa awali.
Akitoa uamuzi huo jana Jumatano, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ritha Tarimo alikubaliana na hoja za wakili wa wasanii hao akisema kuwa kifungu kilichotumika kufungua maombi hayo hakihusiki na nafuu walizokuwa wanaziomba.

AUDIO:S KIDE - SILI KWENU



VIDEO:SELEBOBO - DON'T CARE



G.NAKO:: BAADA YA COVER YA SEDUCE ME YA ALI KIBA, ANAZUNGUMZIAJE UTIMU?

Msanii wa kundi la Weusi, G Nako ameelezea mafanikio ya cover ya ngoma Seduce Me ya Alikiba aliyofanya.

G Nako ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Energy’ amekiambia kipindi cha Clouds E kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa lakini mambo ya u-team katika muziki hayataki.
“Kwanza kabisa sitaki masuala ya ma-team, kuna vitu kidogo yanakuwa yanatuwekea mipaka, mambo ya team yakae mbali halafu muziki mzuri ndio uongee lakini so far mapokezi ni makubwa” amesema G Nako.
G Nako anaungana na producer Man Water na wasanii wengine mbali mbali ambao wamefanya cover ya ngoma hiyo.


BY MPIKO JUNIOR


VIDEO:SHAYDEE FT WIZKID - MAKE SENSE



ENOCK BELLA AMEFUNGUKA KUHUSU KUFUNGA NDOA

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Enock Bella aliyekuwa member wa kundi la Yamoto Band amefunguka taarifa zinazodai amefunga ndoa.

Muimbaji huyo akizungumza na BEST DJ'S EVER TZ amesema si kweli amefunga ndoa kama inavyozungumzwa na picha kuonekana ila itakafika wakati atazungumza.
“Kwa sasa hivi nitadanganya siwezi kuzungumzia hilo suala, kuna wakati nitazungumzia tu ila kuna vitu fulani naviweka sawa. Hapana siwezi kusema nimefunga ndoa au sijafunga ndoa” amesema Enock Bella.
Japo wasanii wenzake aliokuwa nao Yamoto Band, yaani Aslay, Beka Flavor na Maromboso walionekana kumpongeza Bella kupitia mitandao ya kijamii kwa kuashiria amefunga ndoa.

BY MPIKO JUNIOR

Wednesday, October 25, 2017

AUDIO:BARAKA THE PRINCE - SOMETIMES



AUDIO:RICH MAVOKO FT PATORANKING - RUDI





NEWS:BAADA YA "UPO HAPO",MWANA FA,AY NA FID Q NI KUNDI?JIBU HILI HAPA


Baada ya Mwana FA, AY na Fid Q kuachia ngoma yao mpya ’Upo Hapo?’, wameeleza iwapo wameunda kundi lao.
Rapper Mwana FA ambaye amechana vilivyo katika verse ya kwanza ya ngoma hiyo amesema umoja huo hauwezi kutengeneza kundi la watu watatu kwani patachimbika.
“Hili haliwezi kuwa kundi kama ulivyoona video ilivyoisha watu wamebadilikiana mwishoni, haiwezi kuwa kundi kila mtu mbabe, kuwa kundi labda kwa dua zenu lakini sisi kama sisi sioni kundi” Fid Q alimalizia.
Upo Hapo? ni ngoma ya kwanza kuwakutanishwa wasanii hawa watatu kwa wakati mmoja, hapo awali Mwana FA alikutana na Fid Q katika remix ya ngoma ya Nako 2 Nako Soldiers ‘Mchizi Wangu’, wakati AY amekutana na Fid Q katika ngoma kama vile Jipe Shavu, Ujio wa Verse Moja na Shimo Limetema.

NEWS:MSANII ROSA REE AONDOKA 'THE INDUSTRY'


Rapper Rosa Ree amefunguka ishu ya kuondoka katika label ya The Industry.Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow’ amesema mkataba wake na label hiyo ulimalizika na hakuongeza tena, hivyo hivi sasa anaendelea na watu waliokuwa akifanya nao kazi toka awali.

NEWS:SHOW ZA MIKOANI NA BIASHARA NJE YA NCHI ZIMENIPUNGUZIA KIKI - HARMORAPA



Msanii muziki Bongo aliyekuja kwa kasi na kupotea, Harmorapa amedai hajaishiwa kiki kama wengi wanavyodai.Harmorapa ameeleza kuwa ukimya wake unasababishwa na biashara anazofanya nje ya muziki pamoja na show zake za mikoani ambazo amekuwa akifanya mara nyingi.
“Nipo bize sana na mishe nyingine nje ya muziki, namaanisha mimi ni mfanyabiashara, so huwa mara nyingi nasafiri, mara nyingi huwa napiga tour zangu mikoani na project zangu za muziki zipo kama kawaida” amesema.
Ameongeza kuwa kutokana na hilo ni vigumu sana kumkuta Dar es Salaam kwani anakuwa bize sana.