Thursday, November 16, 2017

NEWS:POST YA AFANDE SELE KUMSEMA KANUMBA STEVE NYERERE AMSHUKIA

Msanii wa Filamu Bongo, Steven Nyerere amefunguka kufuatia kauli ya msanii Afande Sele aliyoitoa hivi karibuni kuhusu Marehemu Steven Kanumba mara baada ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii huyo.
Hivi karibu baada ya hukumu hiyo Afande Sele aliibuka na kuandika ujumbe wa kumshtumu Kanumba kwa kitendo cha kutembea na Lulu wakati akiwa bado mdogo, huku akieleza hakushiriki kivyovyote katika msiba wa msanii huyo ingawa alikuwepo Dar kwani hakutaka kuvaa joho la unafki.
Sasa Steve Nyerere katika mahojiano na E-Newz ya EATV amesema muda mwingine wasanii wawe na busara kwa kile wanachokiongea kwani Watanzania wanawaangalia na kuwapima kwa kauli zao.
“Usikurupuke tu, nakumshutumu Marehemu, yaliyopita sisi mbele tungange yajayo. Tunapotaka kufanya kitu jiangalie kwanza, halafu sema mimi ninayeongea jamii nje ninayoingoza naifundisha nini, kuna vitu vingine vinaongelewa hapa ni uchochezi tu, ni uchochezi wa kuua sanaa, mbaya sana” amesema.
Ameongeza kuwa kwa sasa kila mmoja anataka kufukua jambo hilo na wengine wanataka kupata umaarufu kupitia hilo. “Wengine mastaa wa zamani wanataka kujifanya wanalijua kuliongelea hili ili nao wachipukie hapo hapo” amesisitiza.

NEWS:NDIKUMANA AZIKWA KWAO NCHINI RWANDA MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA


Wachezaji wa timu ya Rayon Sports Ismailla Diarra (kushoto) na Tidiane Kone (kulia),wakiwa wamebeba mwili wa marehemu  Hamadi  Ndikumana Katauti kutoka nyumbani kwake Nyakabanda kwenda katika Msikiti Qaddafi uliopo Nyamirambo, Rwanda na baadaye walifanya mazishi jana jioni.
                    

Baba mzazi wa Ndikumana baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa mwanae, Ndikumana akitokea burundi.
Mama mzazi wa Ndikumana akisadiwa amebebwa baada ya kufika Nyumbani kwa mwanae Rwanda akitokea Burundi.
Majirani wakiwa wanalia.
Watoto wakiwa barabarani kuaga mwili wa Ndikumana wakati ukipelekwa katika Msikiti wa Qaddafi  uliopo Nyamirambo, Rwanda.
…Safari ya Kupeleka mwili wa marehemu msikitini ikiendelea.
Ndugu wa Ndikumana akilia kwa uchungu.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa barabarani wakati wa kusindikiza mwili wa marehemu
Mwili wa nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Hamadi  Ndikumana Katauti (39)   amezikwa jana kufuatia kufariki  nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi,  nchini Rwanda katika makaburi  yaliokuwepo kwenye mji wa Nyamirambo, Rwanda.


Ndikumana ambaye  alikuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irine Owoya amezikwa na mamia ya wadau wa soka nchini humo wakiwemo mashabiki wa klabu ya Rayon  Sport ambayo alikuwa akifanyia kazi kama kocha msaidizi.

NEWS:MENEJA WA DIAMOND ASEMA HANA 250 ZA KULIPA,AJIANDAA KISAIKOLOJIA KWENDA JELA

Dar es Salaam. Wakati siku 14 zilizotolewa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd, kwa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection Limited kutekeleza amri ya Mahakama zikikaribia kuisha, Hamis Taletale (Babu Tale), amejitetea huku akidai kuwa anajiandaa kisaikolojia kwa kifungo.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnum, pamoja na nduguye Iddy Taletale ni wakurugenzi na pia wanahisa wa kampuni hiyo.
Februari 18, 2016, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliiamuru kampuni hiyo kumlipa fidia ya Sh250 milioni Mhadhiri wa Dini ya Kiislam Sheikh Hashim Mbonde, kwa kutumia kibiashara mahubiri yake bila ridhaa wala makubaliano.
Babu Tale amekiri kupokea taarifa hiyo ya Yono, lakini akasema kuwa yeye hajui chochote kuhusu madai hayo, kwani hakuwahi kujihusisha na kampuni hiyo na kwamba hana cha kufanya bali anawasubiri kuona Yono hizo siku walizopewa ili waone hatua zitakazofuata.
“Lakini mimi nasema sijamdhulumu huyo mzee wala sijawahi kufanya naye biashara. Kwa kuwa hiyo ni amri ya Mahakama sawa sina cha kufanya, kama watasema tulipe nitaeleza uwezo wangu maana mimi sina uwezo huo wa kulipa hizo Sh250 milioni,” amesema na kuongeza:
“Kwa hiyo cha kufanya ni kujiandaa tu kisaikolojai hata kama ni kufungwa, kwani hata kina Mandela (Nelson) walifungwa jela hivyo hivyo.”
Amesema kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa na ilikuwa ikimilikiwa na kaka yao Abdul Taletale (marehemu kwa sasa) kwa asilimia miamoja na kwamba baada ya kufariki kampuni hiyo haikuendelea na mali zake zote zilipotea kwani zilidhulumiwa.
Amesema kuwa japo anatajwa kama mhusika lakini hakuwahi kuwa mkurugenzi, mwanahisa wala kujihusisha kwa namna yoyote na kampuni hiyo na kwamba hakuona taabu kwani hakujua kama kuna siku yatatokea matatizo kama haya.
Ameongeza kuwa alifahamu kuwepo kwa kesi hiyo baada ya kaka yao kufariki, ambapo wakili wa mdai alimpigia simu akimtaka afike mahakamani, lakini yeye alipuuza kwa kuwa alijua si mhusika.
Kwa mujibu wa hukumu ya kesi ya msingi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, Juni 6, 2013 Sheik Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo, kutumia kazi zake za mawaidha, kwa kuzalisha, kurekodi na kuzisambaza na kugawana faida ya mauzo.
Hata hivyo, baada ya kukamilisha kurekodi masomo saba, kampuni hiyo ilimkatia mawasiliano hadi alipobahatika kukutana na ofisa mmoja wa kampuni hiyo, Adam Waziri ambaye alimweleza kuwa wamesitisha mpango huo.
Lakini Agosti 9, 2013, wakati mdai akiendesha mhadhara Bahi Dodoma, alibaini kuwa DVD za masomo yake zilikuwa zikiuzwa sokoni Dodoma na katika mikoa mbalimbali, bila ridhaa yake wala makubalino ndipo akafungua kesi hiyo. 

AUDIO:MR NANA FT TIMBULO - KWAHERI



Tuesday, November 14, 2017

NEWS:MRISHO MPOTO AMJIBU AFANDE SELE BAADA YA KUMSEMA KANUMBA

Hapo jana msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael (Lulu) kuhukumiwa miaka 2 jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake wa filamu, Steven Kanumba. Msanii Afande Sele aliibuka na kuandika ujumbe wa kumshtumu Kanumba kwa kitendo cha kutembea na Lulu wakati akiwa bado mdogo.
Afande sele alienda mbali zaidi kwa kueleeza kuwa aliumia zaidi baada ya matatizo aliyoyapata Lulu kupitia Kanumba, hivyo hata hakushiriki kivyovyote katika msiba wa msanii huyo ingawa alikuwepo Dar kwani hakutaka kuvaa joho la unafki.
Sasa leo hii Msanii Mrisho mpoto ameiibuka na kupinga vikali kile alichoandika Afande Sele, kupitia ukurasa wake wa Instagram Afande Sele ameandika yafuatayo;
Kaka yangu Afande Sele.. Mfalme wa maandishi…!! @afandeselekingWewe ni Kaka yangu na ni mwandishi ambae sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako …Leo nna mambo kadhaa kidogo kwako Kaka yangu…. Nimesoma maandishi kwenye ukurasa wako zaidi ya mara 30 Huku nikiyarudia rudia mara Kadhaa…ningependa kujua vitu Vichache kabla ya hoja yangu ya msingi kuiweka mezani…ile Barua ulimwandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie? Au ulitaka wanaokwenda nyuma yake wamfikishie? ulitaka waliopo wajifunze kupitia walaka wako? Mbona nimepata kusikia Marehemu huwa halaumiwi kwakua hana uwezo wa kijitetea? Umesema ulikuwepo Sinza wakati wa msiba na hukutaka kusogea wala kuzika kwakua unasema wewe siyo mnafiki kama watanzania waliokwenda kuzika… ikiwa watu wote wangekataa ile Maiti ingekuaje? Nini Hasa lengo la Movies za Kibonge kuziita Maigizo yanayowekwa Kwenye Kanda? una ugomvi na Bongo Movies au uliandika ukiwa kwenye Jazbda kidogo….!! Mimi ndugu 

NEWS:DIAMOND ATAJA BIASHARA INAYOMLIPA ZAIDI KATI YA KARANGA NA PAFYUM


Inafahamika kuwa msanii wa muziki Bongo Flava, Diamond Platnumz miongoni mwa biashara anazomiliki ni Chibu Perfume na Diamond Karanga, sasa ametaja ipi inamlipa kati ya hizi mbili.
Hivi karibuni akiwa katika media tour nchini Uingereza aliulizwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ni biashara ipi inamlipa zaidi na jibu lake lake lilikuwa; ‘Off course, Diamond Karanga’.
Katika hatua nyingine alizungumzia kinachomsukuma zaidi kufungua biashara mbali mbali kwa kusema kuwa anataka kutumia muziki wake katika njia ya kujinufaisha hata pale atakapoacha muziki.
“Unaweza kuwa mwanamuziki lakini ukaweza kufanya vitu vingine katika misingi bora ukatengeneza ajira kwa wenzako ukatengeneza kitu ambacho hata kesho na kesho kutwa usipoweza kuimba ukaweza kupata riziki na familia yako ikanufaika” amesema Diamond.

NEWS:JIBU LA VANESSA MDEE IWAPO WAMERUDIANA NA JUX


Baada ya taarifa kuwa nyingi zikidai Vanessa Mdee na Jux kurudiana, hatimaye Vanessa amejibu ukweli wa suala hilo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Bounce’ amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa hawajarudiana bali kilichopo sasa ni urafiki tu.
“Kitu ambacho nyie hamjui Jux ni mshikaji wangu ni mtu ambaye tunapatana na kufanya kazi pamoja hata vitu vingi ambavyo ni nje ya sekta ya muziki Jux anasapoti, hatuwezi kuanza kugombana na sasa hivi, tunakuwa tunaharibu biashara” amesema.
Vanessa na Jux walikuwa wapenzi na kipindi cha mahusiano yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu pamoja na kushirikishwa katika ngoma ya Nikki wa Pili ‘Safari’.

AUDIO:YCEE - I WISH



VIDEO:JIDENNA - BOOMERANG




AUDIO:AKOTHEE - LALA SALAMA



AUDIO:TEKNO FT WIZKID - MAMA



AUDIO:DAVIDO - FIA




AUDIO:WIZKID FT TY DOLLA $IGN - DIRTY WINE



AUDIO:TY DOLLA $IGN - LAUREN JAUREGUI IN YOUR PHONE



AUDIO:LIAM PAYNE FT QUAVO - STRIP THAT DOWN