Friday, October 20, 2017

AUDIO:WIZKID - ONE MORE DRINK[hit the road]



VIDEO:EDDY KENZO - NDI BYANGE


AUDIO & VIDEO:MWANA FA,AY & FID Q - UPO HAPO


AUDIO:G NAKO - SEDUCE ME [cover]



NEWS:DIAMOND AZUNGUMZIA COLLABO YAKE NA RICK ROSS


Mkali wa muziki wa Bongo Flava, Diamond ameeleza mambo machache kuhusu kolabo yake na rapper wa Marekani, Rick Ross.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Hallelujah’ ameiambia Coconut Fm kuwa ngoma hiyo ni yake Rick Ross kashirikishwa tu.
“Ni wimbo ni wangu mpya nimemshirikisha Rick Ross, kusema wimbo unaitwaje hiyo bado” amesema Diamond.
Katika hatua nyingine amezungumzia ngoma yake ‘Hallelujah’ aliyowashirikisha Morgan Heritage kwa kusema ngoma hiyo alikuwa ameshafanya verse moja na chorus, hivyo walichofanya kundi hilo ni kutuma verse yao tu na mchezo ukawa umeisha.

NEWS:WEMA AFUNGUKA MADAI YA KULALA KWA DAIMOND PLATINUMZ MADALE

KWA mara ya kwanza baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ameanika ukweli juu ya madai mazito kuwa amekuwa akienda kulala nyumbani kwa mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva huko Madale-Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar.
Katika mahojiano juu ya skendo hiyo, Wema alisema kuwa, hakuna jambo linalomuumiza kama ishu hiyo ya kuambiwa huwa anakwenda kulala Madale kwa sababu hajawahi kufanya hivyo hata siku moja, lakini pia huko Madale, anakumbuka alishawahi kwenda wakati nyumba ndiyo kwanza inajengwa na hakuna aliyekuwa akiishi huko.
“Unajua kuna habari nyingine zinaweza kukushangaza sana. Kwenye kumbukumbu zangu Madale nilikwenda wakati nyumba inajengwa kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini siku hizi za karibuni, sijawahi kukanyaga huko.
“Mimi huwa sielewi watu wanapokuwa wanazungumza hivyo vitu inakuwaje, yaani nashindwa kabisa kujua,” alisema Wema.
Wema aliendelea kusema kuwa, watu wakiwa wanajaribu kutengeneza maneno kama hayo ni tatizo kwa sababu zilipendwa wake huyo tayari ana uhusiano na mtu mwingine na wanaendelea na maisha yao hivyo kusambaza uvumi huo ni kumuumiza mwanamke ambaye yuko naye sasa hivi, jambo ambalo siyo zuri.
“Watu wanashindwa kuelewa kwa sasa kila mtu ana uhusiano wake hivyo kusema vitu kama hivyo ni kuharibiana uhusiano ambao unaendelea kwa hivi sasa kwa kila mmoja na hakuna kitu kibaya kama mtu kuvunja uhusiano wake kwa maneno ya kusikia ambayo hayana ukweli,” alisema Wema.

NEWS:DAKTARI WA KANUMBA NAE ATOA USHAHIDI WAKE MAHAKAMANI


Dar es Salaam. Daktari Paplas Kagaiya aliyekuwa akimtibu msanii maarufu wa fani ya uigizaji filamu nchini, Steven Kanumba ametoa ushahidi Mahakama Kuu akieleza hali aliyoikuta alipokwenda nyumbani kwa msanii huyo.
Mbali na Dk Kagaiya, askari Polisi aliyemtia mbaroni msanii wa kike Elizabeth Michael, maarufu Lulu, pia ametoa ushahidi mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 20,2017.
Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kosa analodaiwa kulitenda Aprili 7,2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Kanumba.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi kutoa ushahidi, Dk Kagaiya amesema alipofika nyumbani kwa Kanumba alikuta akiwa ameanguka na alimpima kiwango cha sukari na shinikizo la damu.
Amesema kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo, hivyo alishauri Kanumba apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dk Kagaiya amesema daktari katika kitengo cha dharura Muhimbili alipompima Kanumba aliwaeleza alikuwa tayari ameshafariki dunia.
Baada ya kupewa maelezo hayo, amesema walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Selander Bridge.
Shahidi huyo alipoulizwa na wakili wa Lulu, Peter Kibatala kama kuna vitu vyovyote alivyoviona eneo la tukio chumbani kwa Kanumba, ikiwemo chupa ya pombe alisema hakutambua chochote.
Katika hatua nyingine, askari Ester Zefania kutoka Kituo cha Polisi Msimbazi akitoa ushahidi amesema alikwenda kumkamata Lulu alfajiri, eneo la Bamaga kwa msaada wa Dk Kagaiya, ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa simu.
Akijibu swali la wakili Kibatala kama alimpeleka Lulu hospitalini kwa matibabu, shahidi huyo amesema ni kweli alimpeleka hospitali.
Hata hivyo, Zefania amesema Lulu hakumueleza kuwa alipigwa na Kanumba na wala hakuona majeraha. Alijibu hayo baada ya kuulizwa swali na wakili Kibatala.
Zefania amesema aliagizwa na mkuu wake wa kazi ampeleke Lulu hospitalini lakini hakujua alikuwa ana matatizo gani.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika itaendelea Jumatatu Oktoba 23,2017 kwa upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi wake.

VIDEO:VICTORIA KIMANI FT R CITY - CHINA LOVE



AUDIO:RICK ROSS - TIPTOE'N



AUDIO:JUMA NATURE - KUKAA NYUMBANI



VIDEO:FUTURE FT JO RODEO - COME WITH ME



VIDEO:FALZ - LA FETE



AUDIO & VIDEO:MR P - COOL IT DOWN

https://cloudup.com/files/iVmoS9B2Fzl/download

VIDEO:SUNKANMI - YOU

https://cloudup.com/files/ik-YuGG2tus/download

VIDEOJ:SISTERS - NIPOKEE


AUDIO & VIDEO:HARMONIZE - NISHACHOKA


Wednesday, October 18, 2017

AUDIO:SHAYDEE - HOLD ME TIGHT



AUDIO:DJ SNAKE & MAJOR LAZER FT ELLIE GOULDING - TAKE ME WITH YOU



ALIKIBA AELEZA UMUHIMU WA ELIMU KWA WASANII 'ACHANA NA WANAOIMBA UJINGA'


Hitmaker wa ngoma Seduce Me Alikiba amezungumzia umuhimu wa msanii kuwa na elimu.
“Unajua ubongo wako ukiwa active utaweza kufikiria vitu vya msingi zaidi, achana na watu wanaoimba ujinga, ni kwa sababu tu ya talent lakini elimu ni ya muhimu sana kwenye kila kitu,” amesema Alikiba.
Katika mahojiano Alikiba ameeleza kuwa msanii akiwa na elimu kutamfanya kuweza kufikiri kwa undani zaidi na kumfanya yule anayemsikiliza kutambua msanii husika ni wa namna gani.
“Ukiwa na elimu kama wewe ni msanii ni rahisi kuonyesha watu ubongo wako ukoje, kwa sababu mkasa na visa vipo na maneno yapo lakini utamfanya mtu afikirie huyu alifikiria nini” amesema.
Alikiba bado anafanya vizuri na ngoma Seduce Me ambayo hadi kufikia sasa inaviews milioni 6.9 katika mtandao wa YouTube na ahadi yake ni kuwa ikifikisha views milioni 10 atatoa ngoma mpya.

Tuesday, October 17, 2017

NEWS:GIGY MONEY ADAI HEMEDY PHD SIO LEVEL ZAKE "HANA HELA"

Video Vixen Bongo aliyeamua kutumbukia katika muziki, Gigy Money amedai msanii Hemedy PhD siyo level zake kwa sababu hana fedha.
Kauli ya Gigy Money inakuja baada ya hapo awali kuripotiwa kupishana kauli kwa wawili hao na Hemedy alipoulizwa na kipindi cha The Playlist cha Times Fm alijibu hawezi kumzungumzia Gigy.
Gigy Pia amesema kuwa yeye kwanza hamjui Hemedy na hana hadhi ya kuongea na yeye. “Hawezi kuwa na hadhi ya kuniogelea mtu kama mimi kwa sababu hana hela”, amesema.
Hemedy na Gigy wote wanajihusisha na ‘vitu’ viwili katika tasnia ya burudani Bongo, Gigy anafanya muziki na video vixen, Hemedy muziki na uigizaji.

AUDIO:JYGGA LO FT BECKA TITLE - HAWANIWEZI



NEWS:WEMA SEPETU:UMAARUFU UNANI "COST"

MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Wema Sepetu, analia na umaarufu mkubwa alionao kwani umemfanya kushindwa kufanya vitu vingi ambavyo kama binadamu, na yeye alitamani kufanya.
Akiwa hajawahi kupanda daladala kwa miaka 11 sasa, tangu alipovikwa taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema al-isema akiwa ndani ya gari lake barabarani, hujisikia raha sana kuona watu wakiwa wamepanda usafiri huo, wakiwa wanazungumza na kucheka, kitu ambacho anakimiss sana, lakini hamna namna anayoweza kufanya.
“Unajua kiukweli kabisa natamani mno kupanda daladala, k w a sababu hata mimi ni binadamu, kuna kipindi natamani kupanda gari kutoka kwangu mpaka Kariakoo au mpaka Mbagala, lakini unafikiria utakapopanda itakuwa ni vurugu na siyo starehe tena, huu umaarufu kwa kweli unani-’cost’ sana wakati mwingine,” alisema Wema.

AUDIO:RADIO & WEASEL FT DJ MADENGO - THERE SHE GO



AUDIO:KISS JOE - GANG STAR(Produced by RAXY MOE) EMPIRE MUSIC [www.bestdjsevertz.blogspot.com]