Thursday, January 4, 2018

NEWS:CHIN BEES NDANI YA SKENDO MPYA YA PICHA ZA UTUPU




Msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri kwenye mitindo ya Trap, Chin Bees baada ya kupata skendo kwenye mitandao ya kijamii kwa kusambaa picha akiwa mtupu na mwanamke chumbani, hatimaye amekiri picha hizo zilisambazwa na watu wasiomtakia mema,kwani alikuwa amepoteza simu yake.
Chin Bees alisema kwamba picha iliyosambaa mitandaoni kweli ilikuwepo kwenye simu yake na huyo mwanamke aliwahi kuwa mpenzi wake lakini hakufanya kusudi kuziweka mitandaoni kama jinsi ambavyo watu walivyoanza kumshtumu na kumwambia anatafuta kiki.
Hiyo picha iloyosambaa kwanza sijajua ni nani aliyeisambaza kiukweli ila sio mimi na huyo dada sipo nae tena kwenye mahusiano, na hayupo hata Tanzania. Lakini ninachofahamu nilipoteza simu yangu muda kidogo nilikuwa kwenye bata  moja hivi. Mimi nimefanya kazi zangu za muziki mpaka leo sijatumia kiki sasa kwanini ijekuwa leo” Chin Bees.
Pamoja na hayo Chin Bees amesema kwamba baada ya kutumiwa picha hizo alilazimika kumtafuta mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu kusambaza picha hizo lakini pia alikanusha.
Hii ni skendo ya kwanza kwa Chin Bees kuanikwa mitandaoni kwa kusambaa picha zake za utupu akiwa na mwanamke tangu kuanza safari yake ya muziki.

NEWS:RAY C ATOA KALI YA MWAKA


Msanii Ray C amefunguka na kumuomba Rais Magufuli asaidie kupatikana sheria ambayo itaweza kusaidia wanawake na mabinti wa Tanzania kuolewa kwa haraka kwani anadai bila wanaume kulazimishwa wataendelea kuwachezea mabinti tu.
Ray C amedai kuwa endapo kukiwa na sheria ya kuzuia mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke kabla ya ndoa itasaidia sana wanaume kuoa na kupelekea tatizo la mabinti kutoolewa kupungua.
“Mzee mimi na shida moja, hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili. Naomba upitishe sheria hakuna mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila cheti cha ndoa wapelekwe wote Segerea. Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe” alisema Ray C
Akiongea Ray C amesema kuwa ameamua kuomba jambo hilo kwa kuwa amekuwa akishuhudia wanawake wengi wakiishia kuchezewa na kuachwa pasipo kuolewa lakini anadai kama kukiwa na sheria hiyo wanaume watakuwa na nidhamu na kunyooka maana watalazika kuoa tu.