Saturday, November 4, 2017

NEWS:HARMORAPA NA YEYE KUFUATA NYAYO ZA DOGO JANJA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa ambaye hakauki kwenye mitandao kwa vitendo vyake vya kiki, amesema na amini naye ipo siku atatimiza ndoto zake na kumuoa Wema Sepetu kama alivyofanya Dogo Janja kwa Uwoya.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmorapa ameandika ujumbe akisema kwamba hatokuja kukata tamaa juu ya ndoto yake ya kumng’oa ‘Tz Sweetheart’Wema Sepetu na hatimaye kumuweka ndani kama mke wake.
“Naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kuwa kweli, sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja, naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake, nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu, ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini, kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia… One day you will be mine Wema Sepetu”, ameandika Harmorapa.

NEWS:ZILIPENDWA WA UWOYA AMTUMIA UJUMBE DOGO JANJA


 Mwanamuziki na aliyewahi kuwa mpenzi wa muigizaji Irene Uwoya, Msami Baby amempongeza msanii mwenzake Dogo Janja kwa kufunga ndoa na muigizaji huyo huku akiwasifu kwamba wameweza kuwabadilisha watu kuhusiana na umri.
Msamii ametoa pongezi hizo leo kwenda kwa wawili hao baada ya Dogo Janja kukiri kwa kinywa chake kwamba tukio linaloonekana kwenye picha mbalimbali siyo kiki kama watu wanavyodhani bali ni ndoa kweli.
Msamii ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba  “Ndoa ni jambo la kheri sana, pongezi kwako Dogo Janja na Irene Uwoya mmefanya watu wajue umri ni ‘number’ tu ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi” aliandika  Msami
Msami aliwahi kuwa kwenye mahusiano na muigizaji Irene Uwoya ambapo karibuni alipokuwa kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa kila Ijumaa alipoulizwa kuhusu mahusiano yake na Uwoya alidai walishaachana na kudai kwamba Uwoya ndiye aliyemtongoza mpaka kufikia kuwa wapenzi.

AUDIO:MATONYA - KITUNZE



VIDEO:DJ DAVIZO FT G - NAKO - KINOMA NOMA


Wednesday, November 1, 2017

AUDIO:MIMIMARS - SITAMANI

https://my.notjustok.com/track/download/id/287153/by/odeJO_6OJW

VIDEO:CASSPER NYOVEST - BABY GIRL



AUDIO:MR NICE - YAYA



NEWS:KEISHA AZIDI KUWACHANGANYA WATU KUHUSU HARUSI YA DOGO JANJA NA IRENE UWOYA


Gumzo jingine kuanzia weekend iliyopita ni taarifa za ndoa ya Msanii Dogo Janja ikidaiwa kwamba kamuoa Mwigizaji Irene Uwoya ambapo tayari wawili hao waliandika kwenye mitandao yao ya kijamii kuonyesha kwamba ni kweli wameoana.
Pamoja na hayo leo Msanii wa Bongofleva Keisha ambae alionekana kwenye picha ya pamoja siku ya tukio ameandika maneno ambayo yameonekana kuwachanganya watu baada ya kuonyesha kwamba ile ilikua ni video na itaachiwa hivi karibuni hivyo akawashukuru kina Dogo Janja kwa kuhudhuria

Tuesday, October 31, 2017

NEWS:THE WEEKND NA SELENA GOMEZ WAACHANA RASMI


Staa wa Pop The Weeknd na Selena Gomez wameachana rasmi baada ya miezi 10 kwenye mahusiano  na taarifa hizi zimethibitishwa na mtandao wa PEOPLE.
Hivi karibuni Selena Gomez ameonekana kurudia urafiki wake na pop staa kutoka Canada ambaye pia ni Ex wake Justin Bieber.
Hivi karibuni Selena Gomez alionekana akipata chai ya asubuhi na Justin na weekend hii walionekana pamoja kanisani.
Hivi karibuni Selena alipotea kwenye macho ya watu baada ya kufanyiwa upasuaji wa FIGO
Fahamu kuwa familia ya Selena haiko sawa na Justin kutokana na jinsi alivyomtesa mtoto wao miaka kadha iliyopita wakati wako pamoja mpaka kuachana

VIDEO:FABOLOUS,VELOUS,CHRISS BROWN - FLIPMODE



NEWS:KOLABO YA REMY MA NA LIL KIM NI DIS KALI KWA NICK MINAJI,DILI KUBWA ALILOPATA REMY MA,VIKO HAPA

Rapa Remy Ma asaini mkataba mkubwa na lebo ya Columbia Records na imeripotiwa kuwa anajipanga kutoa Diss nyingine kwa Nicki Minaj atakayo mshirikisha Lil Kim.
Wimbo huo umetajwa kuwa ni ‘Wake Me Up’ Ft Lil’ Kim na tayari wamefanya video ya wimbo huo.
Baada ya mashairi yanayomlenda Nicki Minaj ni pamoja na “That crown, I’m gon’ take that shit / ‘Cause you a clown and homie don’t play that shit.
Mistari hii ina DISS mahusiano ya Nicki Minaj na Nas “I heard he lay that dick, You let them filet that fish / You just met him, how he bae that quick?
Tayari Remy na Nicki wameshabadilishana maneno kupitia Diss track zao “shETHER,” “Another One,” na “No Frauds.”
Kinachosubiriwa kwa sasa ni album mpya ya Remy  Seven Winters, Six Summers,

Monday, October 30, 2017

VIDEO:SARKODIE FT KOREDE BELLO - FAR AWAY



AUDIO:FOBY X MR BLUE - NAOMBA



NEWS:IRENE UWOYA AFUNGUKA BAADA YA KUFUNGA NDOA NA DOGO JANJA


Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake.
Irene Uwoya kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha hilo na kusema kuwa anampenda sana msanii huyo na kudai huyo ndiye mwanaume wa ndoto yake hivyo anafurahi kuona wamefunga pingu ya maisha.
“Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha. Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe” aliandika Irene Uwoya.
Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.

AUDIO:NANDY X ASLAY - MAHABUBA



AUDIO:PITBULL & FIFTH HARMONY - POR FAVOR



AUDIO:MARIAH CAREY - LIL SNOWMAN



AUDIO:YO GOTTI FT CHRISS BROWN - SAVE IT FOR ME



AUDIO:CLEAN BANDIT FT JULIA MICHAEL - I MISS YOU