Monday, November 13, 2017

NEWS:ZARI ALIAMSHA DUDE TENA KWA MOBETO

Siku chache baada kushambuliana kwa maneno kisha ukimya kupita, mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameibuka upya na kumshambulia vilivyo mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Zari aliliamsha dude upya Jumapili iliyopita ambapo alifanya hivyo baada ya kuchokozwa na baadhi ya mashabiki ambao wanaaminika ni wa upande wa Mobeto.
Zari akiwa na mrembo mwenzake aliyeaminika kuwa ni shosti yake, ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alianza kurusha madongo kupitia Instagram katika kipengele cha kurusha matukio moja kwa moja (live).
“Kama yeye ni mwanamke kweli kwa nini ahangaike kulea mtoto? Mimi mwenzake mtu akinizingua nalea mtoto mwenyewe. Ukizalishwa, songa mbele na maisha yako. Tupe nafasi bibi, tupe nafasi. Tiffah anahitaji nafasi, usitubane bane,” alisikika Zari.
Katika video hiyo, Zari alisikika akitema maneno mengi ya kebehi huku shosti yake aliyekuwa amekaa pamoja naye akishadadia kwa maneno ya kumpampu Zari.
Hata hivyo baada ya Mobeto kutopatikana, alipatikana mama mzazi wa Mobeto, ambaye alisema wao kama familia hawasikilizi habari za mitandaoni kwa sasa.
“Yeye awe amesema huko mtandaoni sisi hatujali hayo mambo kwa sasa na wala hayatuhusu, tunaangalia maisha yetu,” alisema mama Mobeto.
Hii ni mara ya pili kwa wawili hawa kutifuana mitandaoni tangu ilipobainika Mobeto kuzaa na mwanaume ambaye pia amezaa na Zari.
Awali, Zari aliposikia mzazi mwenziye amekiri kuzaa na Mobeto, alikinukisha kwa mrembo huyo kisha akakinukisha pia kwa mzazi mwenziye, wakamwagana kwa muda ambapo mrembo huyo wa Kiganda, alisema amemuachia mume Mobeto.
Baadaye Zari na mzazi mwenziye waliweka tofauti zao pembeni, wakaelewana kisha kikapita kimya cha muda mfupi kabla hajaliamsha dude upya juzikati.

No comments:

Post a Comment