Thursday, October 26, 2017

G.NAKO:: BAADA YA COVER YA SEDUCE ME YA ALI KIBA, ANAZUNGUMZIAJE UTIMU?

Msanii wa kundi la Weusi, G Nako ameelezea mafanikio ya cover ya ngoma Seduce Me ya Alikiba aliyofanya.

G Nako ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Energy’ amekiambia kipindi cha Clouds E kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa lakini mambo ya u-team katika muziki hayataki.
“Kwanza kabisa sitaki masuala ya ma-team, kuna vitu kidogo yanakuwa yanatuwekea mipaka, mambo ya team yakae mbali halafu muziki mzuri ndio uongee lakini so far mapokezi ni makubwa” amesema G Nako.
G Nako anaungana na producer Man Water na wasanii wengine mbali mbali ambao wamefanya cover ya ngoma hiyo.


BY MPIKO JUNIOR


No comments:

Post a Comment