Thursday, October 12, 2017

JAGUAR AOMBA RADHI BAADA YA KUPIGANA BUNGENI WIKI HII

Moja ya stori ambayo ilikuwa gumzo kutoka Kenya jana October 11, 2017 ilikuwa ni kuhusu ugomvi uliotokea katika Bunge la nchi hiyo uliopelekea hata Wabunge wawili vijana; Mbunge wa Starehe Charles Njagua Kanyi, maarufu kama Jaguar kuzichapa na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino.
Sasa, Mbunge Jaguar ameomba radhi kwa wapiga kura wake na Wakenya kwa ujumla kutokana na tukio hilo.
Wawili hao walifikia hatua hiyo wakiwa ndani ya Bunge Jumanne jioni baada ya Owino kusema Rais Uhuru Kenyatta ni kiongozi anayeilea Serikali, lakini mwisho wake utafika karibuni.
Baada ya kutoelewana katika ukumbi wa habari ndani ya Bunge, walianza kurushiana maneno huku Owino akisisitiza hatotambua uhalali wa Rais Kenyatta ambapo alinukuliwa akisema;>>>”Jaguar, huwezi leta ushenzi. Hii Kenya ni ya watu wote.”
Kwa upande mwingine, Jaguar alisikika akisema:>>>”Babu, lazima umheshimu Rais, kama hutaki, tutakushughulikia.”
>>>”Kilichotokea (Bungeni) kilikuwa kibaya sana. Nimemsamehe Babu Owino. Nami naomba anisamehe pia. Hata hivyo, nasisitiza kwamba Babu Owino lazima amheshimu Rais. Asimkosee heshima Kiongozi wa Dola – tena –, nitapambana naye.” alisema Jaguar alipokuwa anazungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa habari wa Bunge.

BY MPIKO JUNIOR.


No comments:

Post a Comment