Sunday, January 14, 2018

NEWS | BILL NASS AJIBU OMBI LA NDOA KWA NANDY


Msanii Bill Nass amejibu kauli ya Nandy aliposema kuwa anatamani angekuwa mke wake, na kusema kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani ingawa anaheshimu hisia zake
Akizungumza na mwandishi Bill Nass amesema kwa sasa hawezi kujibu kwa mtazamo positive kwani kufanya hivo kutaharibu mahusiano yake ya sasa, lakini anaheshimu hisia za Nandy.
“Kwa coment yangu kwa sababu mtu ameelezea hisia zake kutokana labda na personality zangu, ila hanijui kiundani, siwezi kujibu in positive ingawa naheshimu hisia zake naheshimu alichokizungumza, lakini kutokana na mahusiano ambayo niko nayo siwezi kufanya move yoyote kwake, naheshimu mahusiano yangu, siwezi kucoment chochote ambacho hakitampendeza mwenzangu na hakitakuwa na mrejesho mzuri kwenye mahusiano yangu, lakini naheshimu hisia zake”, amesema Bill Nas.
Hivi karibuni msanii Nandy alinukuliwa na moja ya chombo cha habari akisema anatamani angekuwa mke wa Bill Nass kwani anamzimia msanii huyo.

No comments:

Post a Comment